TAARIFA ILIYOTOLEWA JANA KUHUSIANA NA UBOMOAJI WA NYUMBA MANISPAA YA KINONDONI
Manispaa
ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi , kama msimamizi na mtekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi,
inakusudia kuendesha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa bila kufuata
taratibu za ujenzi.
Maeneo
yaliyotengwa mijini kwa matumizi ya umma ikiwa ni pamoja na maeneo ya
wazi, njia za miundombinu na huduma nyinginezo za umma, mara kwa mara
hutumiwa vibaya au kuvamiwa na waendelezaji binafsi hivyo kuukosesha
umma manufaa yaliyokusudiwa.
Tamko Na. 6.6.1 la Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995:
i.
Serikali itahakikisha kwamba maeneo yote mijini yaliyotengwa kwa
shughuli za umma yanatumika kwa shughuli zilizokusudiwa na yanalindwa
ili yasivamiwe.
Tamko Na. 8.2.1 la Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995:
ii. Serikali za mitaa zitawajibika kushirikiana na Wizara ya Ardhi kuhakikisha usimamizi mzuri wa ardhi katika maeneo yao.
Sera
ya Taifa ya Ardhi imebainisha sababu inayopelekea Wizara kushirikiana
na Manispaa ya Kinondoni kuendesha zoezi hili la ubomoaji.
Ubomoaji huu utahusisha nyumba zote zilizojengwa
a) Bila kibali cha ujenzi
b) Bila kufuata michoro ya mipango miji
c) Bila kufuata matumizi ya ardhi (maeneo ya wazi)
Zoezi
hili la ubomoaji litaendeshwa na Manispaa ya kinondoni na Wizara ya
Ardhi itasimamia sera za ardhi na taratibu za uendelezaji kuhakikisha
zinafuatwa na kila mmiliki wa ardhi.
Maeneo
ambayo ujenzi wake umekiuka matumizi kusudiwa na yatahusika na ubomoaji
huu ni Mbezi, Tegeta, Bunju, Mwenge na Kinondoni – Biafra. Kazi hii
inatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia jumatano tarehe 18/11/2015
hadi ijumaa tarehe 20/11/2015 |
0 comments:
POST A COMMENT