WAZIRI MKUU MTEULE KASSIM MAJALIWA KUAPISHWA LEO IJUMAA | MASWAYETU BLOG
Breaking News

Thursday, November 19, 2015

WAZIRI MKUU MTEULE KASSIM MAJALIWA KUAPISHWA LEO IJUMAA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Sherehe za kumuapisha Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu Mteule zitafanyika katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Novemba, 2015 kuanzia saa 4.00 Asubuhi.

Sherehe hizo zinafanyika siku moja baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha jina lake kwa kura nyingi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia uteuzi uliofanywa na Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa ratiba ya sherehe hizo, Wageni waalikwa wote wanapaswa kuwasili katika Ikulu ya Chamwino kuanzia majira ya saa mbili asubuhi.


Sherehe hizo zinatarajiwa kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo Marais Wastaafu, Mawaziri Wakuu wastaafu na waheshimiwa wabunge.

Imetolewa na Idara ya Habari MAELEZO

19 Novemba, 2015

google+

linkedin

MASWAYETU EXCLUSIVE BLOG
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0768 260834. Soma Zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    IDADI YA WASOMAJI

    61,119