
Mwigulu Lameck Nchemba Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi akiapa mbele ya Spika Job Ndugai.
Mwigulu Lameck Nchemba Mbunge wa Jimbo
la Iramba Magharibi amezua gumzo Bungeni katika kikao cha Bunge la 11
kilichoketi leo (Jana) asubuhi wakati Spika wa Bunge Bw.Job Ndugai akiwaapisha
wabunge wateule kuwa wabunge rasmi.
Katika zoezi hilo la kuapa ambapo wabunge mbalimbali wamelipitia,kila
Mbunge anafika mbele ya Spika na kupewa kitabu chenye maelezo ya kuapia
ambapo wabunge asilimia kubwa wamekuwa wakisoma ila ilipofika zamu ya
Nchemba imekuwa tofauti ambapo yeye hakukifungua kitabu chenye maelezo
ya kuapia na badala yake kuapa pasipo kusoma kitabuni.
Mara baada ya kumaliza kuapa wabunge walisikika wakimshangilia kwa kumpigia makofi huku baadhi yao wakisema kuwa ‘amekariri’.
Mara baada ya kuapa Nchemba anakuwa sasa ni mbunge rasmi ambapo anaweza kuanza kutekeleza majukumu kama mbunge halali wa jimbo la Iramba Magharibi“Du,amekariri hadi maneno ya kuapia kweli jamaa kiboko” alisikikika akisema mmoja wa wabunge bungeni hapo.
0 comments:
POST A COMMENT