Nyumba Yaanguka na Kuua Wawili Manyoni | MASWAYETU BLOG
Breaking News

Wednesday, November 18, 2015

Nyumba Yaanguka na Kuua Wawili Manyoni



WATOTO wawili, akiwemo mwanafunzi wa shule ya msingi Mkwese wilayani Manyoni mkoani Singida, wamekufa baada ya kuangukiwa na nyumba ya tembe kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kijijini hapo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa Singida, Thobias Sedoyeka aliwataja waliokufa kwenye ajali hiyo kuwa ni Jumapili Mayunga (12) na Masegese Mayunga wakazi wa kitongoji cha Mningaa katika kijiji cha Mkwese wilayani Manyoni.

Sedoyeka alisema mjini hapa jana kuwa ajali hiyo ilitokea juzi baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kunyesha kijijini hapo, hivyo kusababisha nyumba walimokuwa wamelala watoto hao kuanguka na kuwafukia.

Kwa mujibu wa Kamanda Sedoyeka, wazazi wa watoto hao walikuwa wamelala nyumba nyingine jirani na kwamba waligundua tukio hilo mara baada ya kusikia kishindo kwenye nyumba walimokuwa wamelala watoto hao na hivyo kwenda kuangalia kulikoni.

“Mara baada ya kuona watoto wao wamefunikwa na udongo wa nyumba hiyo, walipiga kelele za kuomba msaada kwa majirani na walipokuja juhudi za kuwafukua zilianza lakini kwa bahati mbaya waliwakuta tayari wameshapoteza maisha,” alieleza Kamanda Sedoyeka.

Kutokana na tukio hilo, Sedoyeka ametoa mwito kwa wakazi wa mkoa wa Singida kuchukua hadhari mbalimbali kwenye maeneo yao wakati huu wa kipindi cha masika ambapo mvua kubwa zinaendelea kunyesha na aghalabu, huleta madhara.
 
Habari Leo

google+

linkedin

MASWAYETU EXCLUSIVE BLOG
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0768 260834. Soma Zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    IDADI YA WASOMAJI

    61,109